Aliyewahi Kutajwa Kuwa Adui Wa Taifa, Ateuliwa Kuwa Mkurugenzi Wa Mawasiliano Ya Rais Ikulu

Watu wamekuwa na mitazamo hasi juu ya waandishi wa habari wa kitanzania, wanaofanya kazi na vyombo vya habari vya kimataifa, huku wakienda mbali zaidi na kuwaita wasaliti na watu wasio wazalendo kutokana na kutoa taarifa ambazo zinaonekana kulichafua taifa.

Gazeti la Fahari Yetu la nchini Tanzania toleo la tarehe 21, septemba, 2020 lilichapisha habari yenye kiwa kinachosomeka “maadui wanne hatari kwa amani ya taifa” miongoni mwa waliotajwa katika orodha hiyo ni aliyekuwa mtangazaji wa idhaa ya Kiswahili ya BBC Zuhura Yunusi, huku wakimtuhumu kutumiwa na makundi ya wanahabari ili kuchafua serikali ya awamu ya tano iliyokuwa chini ya hayati Dkt, John Pombe Magufuli.

Watu wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni pamoja na Jeffrey Smith ambaye alituhumiwa kuingilia uchaguzi wa Tanzania kwa kusaidia upande wa aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA Tundu Lisu, Joe Trippi akituhumia kutoa fedha kwa wanasiasa ili kupindua serikali, pamoja na Amsterdam aliyetajwa kuwa anatetea magenge ya waharifu yenye malengo ya kupindua serikali katika mataifa mbalimbali.

Uteuzi wa Zuhura Yunus Leo februari Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza kumteua aliyekuwa mtangazaji wa BBC Bi Zuhura Yunusi kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, akichukua nafasi ya Jaffar Haniu, ambaye ametajwa kupangiwa nafasi nyingine ambayo mpaka sasa haijawekwa wazi. Ikumbukwe kuwa kazi za mkurugenzi ya mawasiliano ikulu ni pamoja na kuratibu utoaji wa taarifa za ikulu, hivyo moja kwa moja atakuwa na taarifa zote za nchi na anamamlaka ya kusambaza taarifa kwa ajili ya kuhabarisha umma ikiwemo vyombo vya habari, Zuhura Atangaza kuondoka BBC Mnamo Januari 14 2022, Zuhura Yunusi alitangaza rasmi nia yake ya kuondoka katika kituo cha utangazaji cha BBC baada ya kufanya kazi katika kituo hicho kwa takribani miaka 14, ambapo alianza kufanya kazi kama mtangazaji wa BBC mwaka 2008.

Imekuwa kama neema kwa watangazaji waliopita katika kituo hicho kupata uteuzi wa nafasi ya ukurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu, miezi michache zilizopita aliyewahi kuwa mtangazaji wa BBC Charles Hilary alitangazwa pia kuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Zanzibar.

Hii inaonesha serikali ya Rais Samia pamoja na Husein Mwinyi wa Zanzibar wamekuwa na imani na waaandishi waliotumikia vyombo vya habari vya kimataifa kutokana na uwezo wao mkubwa katika habari na mawasiliano ya umma.

Je Zuhura Yunusi ni nani Nje ya cheo cha Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu?

Zuhura Yunusi amehudumua kama mwandishi na mtangazaji katika vyombo vya habari tofauti tofauti nchini Tanzania, kabla ya kujiunga na BBC ikiwa ni pamoja na Redio Times FM, Uhuru Fm pamoja na kufanya kazi katika gazeti la serikali la The Citizen.

Sambamba na kazi hizo pia anatajwa kuwa mwanamke wa kwanza kuaminiwa kutangaza katika kipindi cha Dira ya Dunia katika kituo cha habari cha BBC chenye makao yake makuu katika mji wa London nchini Uingereza.

Katika kazi yake ya utangazaji na uandishi alifanikisha kujinyakulia tuzo ya habari ya Isha, baada ya kuandika ripoti juu ya Virusi vya Ukimwi nchini Tanzania mwaka 2002, hivyo tuzo hiyo ilionesha mchango wake wa moja kwa moja katika jamii.

Kama ilivyo kwa watoto wengi kutamani kuwa madaktari katika maisha yao, ata kwa upande wake Zuhura Yunus alitaja kuwa na ndoto ya kuwa daktari lakini mambo yalibadilika hivyo mwaka 2000 ndoto ilibadilika hivyo akatimkia kwnye mtangazaji wa redio.

Akizungumza na Kituo cha habari cha Mwanachi, Zuhura aliweka wazi kuwa, alisoma masomo ya Fizikia, kemia na biolojia, akathubutu kusoma shahada ya kwanza ya wanyama na mimea nchini Uganda, na baada ya kuhitimu alirejea nchini Tanzania akiwa amejiandaa kupata kazi na kuwa daktari, Lakini badala yake alienda kuomba kazi katika kituo cha redio cha Times FM mwaka 2000 baada ya kushauriwa na kaka yake, na akafanikiwa kupata kazi na kufanya kazi kama mtangazaji wa redio badala ya fani ya udaktari aliyoisomea nchini Uganda.

Ikumbuke kuwa Sheria ya habari ya Tanzania inamtaka mtangazaji wa kituo cha redio na televisheni, kuwa na elimu ya mawasiliano ya umma hivyo ilimlazimu kujiendeleza kielimu na kupata shahada ya uzamivu ya mawasiliano ya umma.

CHANZO: Ikulu mawasiliano, Gazeti la Fahari Yetu, BBC Swahili Pamoja na Mwananchi Digital

Enjoyed this article? Stay informed by joining our newsletter!

Comments

You must be logged in to post a comment.

About Author

JOURNALIST