Baada Kuchelewa kwa Miaka Miwili, Hatimaye Chuo Cha Uongozi Cha Mwalimu Nyerere Chazinduliwa Rasmi

Baaada ya ujenzi wa chuo cha uongozi cha mwalimu Nyerere kutokukamilika kwa wakati, hatimaye ujenzi wake umekamilika na kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania akishirikiana na viongozi wa vyama rafiki vya siasa Afrika.

Chuo kilipangwa kukamilika mnamo mwaka 2020, lakini kutokana na sababu ya uviko19 pamoja na mvua kuongezeka, ujenzi ulichelewa hivyo kupelekea kuzinduliwa siku ya yao Februari 23 mwaka 2022.

Chuo hicho kimejengwa kwa udhamini wa chama cha kikomunisti cha China, ikiwa ni maombi ya viongozi wa Afrika kuomba kuwa na chuo hicho kitakachowasaidia makada wa vyama vya siasa kusini mwa Afrika, kuwaandaa makada wa vyama hivyo na kuwapa fikra pana za kiuongozi.

Ikumbukwe kuwa serikali ya CCM inatamba kuwa ya mfumo wa kikomunist ambayo unajulikana kama ujamaa na kujitegemea, hivyo ilikuwa rahisi sana kwa serikali ya China kukubali kufadhili mradi huo mpaka ukamilike.

Katika kukamilisha azima hiyo jumla ya vyama sita viliungana na kuazimia kujenga chuo kimoja huku wakikipa jina la Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere.

Vyama hivyo ni pamoja na CCM cha Tanzania, Frelimo cha Msumbiji, MPLA cha Angola, ZANU PF cha Zimbabwe, SWAPO ya Namibia pamoja na chama cha ANC cha Afrika ya Kusini, hivyo mafunzo yatalenga kwafunzi kutoka katika nchi hizi 6, huku mshirika mkuu akiwa ni China kupitia chama chake cha Kikomunisti

Akizungumza katika uzinduzi huo Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Samia Suluhu Hassan amesema kuwa chuo hicho kitaenda kujibu maswala kadhaa kutokana na namna vyama hivi vinavyosemwa.

Ikumbukwe kuwa baadhi ya vyama vilivyopigania uhuru vimekuwa vikifanyiwa mpango wa kuondolewa madarakani, huku nchi ambazo zimefanikiwa kufanya hivyo zikionekana mashajaa, 

Pia ameongeza kuwa kuna maandiko yanasema kuwa viongozi wapigania uhuru awawezi kuleta maendeleo nchi zetu pia ni watu ambao wamangang’ania madarakani hivyo kupitia chuo hiki, itasaidia kubadilisha mitazamo ya uongozi pia kujibu maswala mengi ambayo yaliandikwa siku za nyuma,

Malengo ya kuanzishwa kwa chuo

Katika hotuba ya Rais Samia amebainisha kuwa, kupitia chuo hiki kitasaisia vijana kufanya tathimini ya maendeleo katika nchi shirika ambazo na Tanzania, Angola, Zimbabwe, Namibia, pamoja na Afrika ya Kusini.

Tathimini hii itasaidia katika kuchochea maendeleo ya nchi kutokana na kuongezeka uwajibikaji miongoni mwa viongozi, huku baadhi ya viongozi wakipewa mafunzo mafupi ambaya tayari yameanza kufanyika katika chuo hicho na kuwatoa viiongozi katika ngazi tofauti tofaut.

Tumeshuhudia vyama tofauti tofauti vikianzisha katika nchi mbalimbali huku vikikosa namna ya kuweka wazi itikadi mahususi ya vyama vyao na kutokueleweka katika jamii, hivyo kupitia chuo cha uongozi itasaidia kupeleka elimu kwa jamii juu ya itikadi tofauti tofauti za uongozi.

Mkono wa China katika Kupambania Uhuru wan chi za kusini mwa Afrika

Msaada wa china kwa vyama vya siasa Afrika ulianza tangu harakati za uhuru, huku wakitoa msaada wa mafunzo ya kijeshi wa wanaharakati wa ukombozi ambayo ilizaa matunda na kusaidi nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania kupata uhuru wake mnamo mwaka 1961.

Hivyo msaada wa serikali ya China katika kujenga chuo hicho, inaonesha mwendelezo wa ushirikiano kati ya chama cha Kimomunist cha China na vyama mbalimbali vya Afrika vilivyoshiriki katika harakati za ukombozi na wa mataifa yao na kuleta uhuru.

Katika sekta nyingi za kimaendeleo, zimekuwa zikiongozwa na misingi ambayo hufundishwa, lakini tumeshuhudia viongozi wengi wakiingia katika siasa kutokana na umaarufu wao, bila kuwa na ubobezi katika maswala ya kisiasa jambo ambalo linapunguza weredi wa kazi huku viongozi wengne wakishuhudiwa wakishindwa kutengeneza sere nzuri za kimaendeleo.

Hivyo ni imani ya watu wengi kuwa kuanzishwa kwa Chuo cha uongozi kitasaidia kuzalisha vijana waliobobea katika maswala ya kisiasa hivyo kuwa chachu katika maendeleo ya vyama vyao na taifa kwa uzumla.

Chanzo: TBC1

Enjoyed this article? Stay informed by joining our newsletter!

Comments

You must be logged in to post a comment.

About Author

JOURNALIST