Mgogoro Kati ya Urusi na Ukraine Ambao Umesababisha Vita inayoendelea Mpaka sasa Uko Hivi...........

Ukraine na Urus ni nchi za Ulaya Mashariki. Kabla ya mwaka 1991, nchi zote mbili zilikuwa ni sehemu ya Umoja wa Kisovieti. Ukraine ni nchi iliyopo Barani Ulaya, idadi ya watu wake inakadiriwa kuwa milioni 44. Urusi ndio nchi kubwa zaidi duniani, idadi ya watu wake ni milioni 144.

Baada ya kuvunjika Umoja wa Kisovieti (Muunganiko wa nchi mbalimbali zikiwemo Urusi na Ukraine huko Ulaya Mashariki) Ukraine iliweka utegemezi na kufanya biashara na nchi za Magharibi ambao ni Marekani na washirika wake. 

Kitendo hiki kimekuwa kikiiudhi Urusi ambayo inaona kwamba Ukraine kuwa karibu na nchi za Magharibi inaathiri usalama wake na maslahi yake.

Mwaka 2014, Rais Viktor Yanukovych wa Ukraine aliondolewa madarakani na kukimbilia uamishoni Urusi. baada ya kutuhumiwa kuwa mshirika mkubwa wa Urusi, na katika utawala wake alifanya mambo mengi kuipendelea Urusi. 

Sasa Baada ya Rais huyo kuondolewa madarakani, Urusi ilivamia na kuiteka sehemu ya Ukraine, Crimea na kuifanya sehemu yake.

Baada ya Yanukovych ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Urusi kuondolewa madarakani Ushirikiano wa Ukraine na Umoja wa Ulaya uliongezeka zaidi na ushirikiano huo umeimarishwa zaidi baada ya Rais wa sasa wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuingia madarakani jambo linamuudhi sana Urusi chini Rais Putin.

Baada ya kuchaguliwa ziara yake ya kwanza ya Rais huyu alitembelea makao makuu ya Umoja wa Ulaya na NATO. na ikumbukwe kuwa Urusi sio mwanachama wa NATO.

Mpango wa Ukrain kujiunga na NATO ni tishio kwa usalama wa Urusi, kwa sababu nchi hizo zimepakana. 

Hofu ni kwamba Marekani ambaye ni mshirika wa NATO anaweza kuweka military base kubwa nchini humo na kuelekeza zana hizo Urusi. 

Sasa Urusi imeamua kuingia vitani ili kuzuia ushirikiano zaidi kati ya Ukraine na Umoja wa Ulaya, NATO pamoja na washirika wao ikisema Ukraine anakiuka mkataba wa Amani na Urusi.

Jana Rais Zelenskyy amesema anajua lengo namba moja la Urusi ni kutaka kumfilisi yeye mwenyewe pamoja na familia yake.

Mpaka sasa watu 137 wakiwemo wanajeshi na raia wa kawaida wa Ukraine wamefariki kufuatia mashambulio ya Urusi katika nchi hiyo. 

Urusi inatajwa kumiliki takribani asilimia 90% ya nuclear, na ni msambazaji mkuu wa gesi huko Ulaya. hivi karibuni alisaini mkataba wa kidiplomasia na China. 

 

Enjoyed this article? Stay informed by joining our newsletter!

Comments

You must be logged in to post a comment.

About Author

JOURNALIST