Ibilisi hutumia sana mbinu hii ya hasira ili kuwatumikisha watu pia mbinu hii ya hasira hutumiwa na wachawi ili kuwachukua watu kuwa misukule. Shetani na wajumbe wake husababisha mtu akasirike yaani wanaweza wakatengeneza mazingira ya kumfanya mtu akwazwe na kukasirika Ili wamnase.mtu anapokasirika tuu tayari anafungua mlango wa mapepo kumwingia na kuanza kumshambulia. Waefeso :4-26.inatufundisha hasira ni asili ya mwanadamu,ukikasirika usitende dhambi na hasira isikae ndani yako kwa muda mrefu ,kwani madhara ya hasira huleta madhara makubwa. ROho ya hasira inahitaji kushughulikiwa kwa maombi makali ya Vita kwani imesababisha uharibifu mkubwa kwenye maisha ya watu. Watu wengi wamefukuzwa kazi kwa sababu ya hasira ,kwa kushindwa kukaa na wafanyakazi wenzao.Na ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu ya kushindwa kuzuia hasirana wengine wameua watu sababu ya hasira. Hupaswi kuipuzia hii roho kwani ni silaha mbaya sana kutoka kuzimu iliyolenga na kuharibu miujiza ya wtu wengi.
You must be logged in to post a comment.