Mtu anayefuatiliwa na hi ROho ni mtu ambaye_: 1.Tatizo likitokea katika eneo la kazi wengine wote watasamehewa lakini yeye peke yake atafukuzwa kazini hata Kama Hana hatia. 2.watu wakiwa wanapita kwenye daraja wengine wote watavuka salama lakini ikifika zamu yake daraja linakatika. 3. Ajali ya basi ikitokea wengine wote watapona lakini yeye peke yake ataumia na hata kufa . 4.Hana kibali popote pale anapokwenda hakubaliki .kwa maana anaweza kuwa na sifa zote za kupata kazi lakini Kila mahali akienda anakataliwa. Hutakiwi kuipuzia hii roho kwani lengo lake ni kukuangamiza kabisa hatima yako. Watu wengi wanaishi maisha ya kuny'ong'onyea na huzuni kwa sababu ya mikosi wanayokutana nayo Kila mara. Jambo la msingi na busara ni kuomba kwa bidii unapogundua kuwa ROho Kama hii inakuduarilia kwani ni hatari kwa maisha yako.
You must be logged in to post a comment.